Wednesday, 6 May 2015

Maelfu wakimbia Niger wakiihofia Boko Haram

Watu wapatao elfu tano wamevikimbia visiwa katika Ziwa Chad kusini-mashariki mwa Niger wakihofia mashambulizi mapya ya kundi la kigaidi la B... thumbnail 1 summary
Watu wapatao elfu tano wamevikimbia visiwa katika Ziwa Chad kusini-mashariki mwa Niger wakihofia mashambulizi mapya ya kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo linaandamwa vikali nyumbani nchini Nigeria.
Wakaazi wa visiwa vya Ziwa Chad wakijiandaa kuondoka Wakaazi wa visiwa vya Ziwa Chad wakijiandaa kuondoka
Afisa wa Umoja wa Mataifa ameliambia shirika la habari la Ufaransa-AFP, kuwa zaidi ya watu 5,000 tayari wamewasili N'Guigmi, mji ulioko kusini-mashariki mwa Niger unaopakana na Chad. Amesema wengine 11,500 wanatarajiwa kuwasili kwenye mji huo. Wiki iliyopita maafisa wa Niger, waliwataka wakaazi wa maeneo ya karibu na Ziwa Chad kuondoka kwenye visiwa hivyo ifikapo jana Jumatatu, ikihofia uwezekano wa Boko Haram kushambulia visiwa hivyo.
Moussa Tchangari, mkuu wa shirila la Niger lisilo la kiserikali, amesema maelfu ya wanaume, wanawake, watoto na wazee, walitembea umbali wa kilomita 50 hadi kuufikia mji wa N'Guigmi. Tchangari amesema watu hao walikuwa wamechoka kupita kiasi, wana njaa na kiu, wakati walipowasili mjini humo.
Hata hivyo, amesema mji huo haukuwa umeandaliwa kwa ajili ya kuwapokea na kuwasaidia maelfu ya watu hao,
Mmoja wa wanawake waliookolewa Mmoja wa wanawake waliookolewa
shutuma ambazo zimekanushwa na maafisa wa serikali ya Niger. Gavana wa Diffa, amesema leo kuwa kila kitu kinakwenda vizuri. Duru za Umoja wa Mataifa, zimeeleza kuwa serikali imeanza kugawa misaada.
Wakati huo huo Kundi la kigaidi la Boko Haram liko katika hatari ya kuvunjika baada ya mvutano kuzuka kati ya wapiganaji na viongozi wa kundi hilo. Inadaiwa kuwa mvutano huo unachochewa na uhaba wa silaha. Mvutano huo unazuka wakati ambapo majeshi ya serikali yanazidi kusonga mbele.

No comments

Post a Comment