Thu May 14 2015
Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Daktari Leonard Subi
Mtu mmoja amekufa na wengine 65 wanaugua ugonjwa wa kuharisha
ulioibuka katika kitongoji cha LUSOLO katika kijiji cha KAGUNGA
wilayani KIGOMA.
Kwa mujibu wa mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Daktari Leonard Subi kukosekana kwa huduma hizo muhimu za kijamii ndiyo chanzo cha kuibuka kwa ugonjwa wa kutabika na kuharisha.
Akizungumzia kuhusu jitahada za kukabiliana na mlipuko huo Daktari Subi anasema tayari wameshapeleka wataalama wa afya katika eneo hilo na kwamba wataalam kutoka wizara ya afya na ustawi wa Jamii pamoja na wa shirika la afya `1Duniani WHO wapo mkoani Kigoma kuongeza nguvu za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Nao baadhi ya waomba hifadhi kutoka nchini Burundi waliopo katika kitongoji cha LUSOLO wameanzisha uratibu wa kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kuchimba mashimo kwa ajili ya kuweka taka ngumu ambazo zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku
tbc, mei 14
No comments
Post a Comment