Head
of India Tanzania Center of Excellence in ICT (DIT), Dr. Amos Nungu
akiwakaribisha wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), wakufunzi pamoja na walimu waliofika
kwenye mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao.Afisa
mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo akimkaribisha Ofisa
anayeshughulikia na masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
(wa kwanza kutoka kushoto) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu kwa
njia ya mtandao kwa walimu wa vyuo vya elimu.Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
akifungua mafunzo kupitia njia ya mtandao iliyoandaliwa na UNESCO
yaliyofanyika jijini Dar. Bi.
Eunice Gachoka kutoka Kenya Institute of Curriculum Development
akijitambulisha kwa walimu (hawapo pichani) waliofika kwenye mafunzo ya
kupitia mtandao. Daudi
Mbona mkufunzi kutoka chuo cha DIT akiendelea kutoa mafunzo kwa baadhi
ya walimu walioudhuria mafunzo ya kupitia njia ya mtandao yaliyofanyika
kwenye chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) hapa jijini
Dar. Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao. Baadhi
ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo. UNESCO imeaandaa mafunzo ya
uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Tehama kwa vyuo
mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu. Mafunzo hayo
yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika katika chuo cha Dar es Salaam
Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa
vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya
Tehama. Hii inatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali
pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini Tanzania hivyo kuona kama kuna
mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama hasa katika
vyuo hivyo. Baada ya kuona kuna mapungufu hayo UNESCO waliamua kuanzisha
mradi uitwao UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wakishirikiana
na vyuo vya elimu hapa nchini Tanzania waliamua kuanzisha mradi huo kwa
malengo makuu matatu ambayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya
ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika Tehama ili
kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya
Tehama ambavyo vitasaidia katika kufundishia na kujifunzia, Afisa
mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo alivitaja vifaa hivyo kwa
kuviorodhesha kuwa ni pamoja na kompyuta, Projecta, na Sola ili
kuhakikisha hakuna tatizo la umeme katika ufundishaji wa masomo hayo.
Kupitia mradi huo wa (CFIT), UNESCO imeandaa mafunzo ya siku tano kwa
walimu wa vyuo vya ualimu kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu hapa nchini
Tanzania ili kuongeza ujuzi na ufanisi katika ukuzaji wa Tehama hasa
kupitia kwenye njia ya mtandao na pia kuendana na wakati kutokana na
mabadiliko pamoja na ukuaji wa matumizi ya Teknolojia Mafunzo haya
yaliyoandaliwa na UNESCO yanafanyika katika chuo cha Dar es Salaam
Institute of Technology (DIT) kwa ajili ya kuwapa elimu kwa baadhi ya
walimu wa vyuo ili kupata uelewa zaidi juu ya Tehama. Wakufunzi wa
mafunzo hayo ni Daudi Mboma ambaye ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya
biashara kutoka (DIT) na Godfrey Haongo kutoka Open University of
Tanzania ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo
tofauti hapa . Waalimu tisa kutoka chuo cha ualimuTabora, waalimu tisa
kutoka chuo cha ualimu Monduli, walimu wanne kutoka chuo cha ualimu
Morogoro, mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson
Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District, pia kuna baadhi ya
watakao pata mafunzo hayo wanatokea Wizara ya elimu ambao wanafanya kazi
kwa ushirikiano na UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa
vyuo vya elimu hapa nchini. Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala
ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya
kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za
kitehama katika taifa la Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa
mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika
ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa
wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya
nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.Na Geofrey Adroph.
Source: Kilimanjaro Official Blog.....................19 mei 2015
Source: Kilimanjaro Official Blog.....................19 mei 2015
No comments
Post a Comment