Tuesday, 19 May 2015

EU yaanzisha operesheni dhidi ya biashara ya wahamiaji

Shughuli za uokozi kwa wahamiaji kwenye mwambao wa Lampedusa, Mei 8 mwaka 2015. Reuters ... thumbnail 1 summary


Shughuli za uokozi kwa wahamiaji kwenye mwambao wa Lampedusa, Mei 8 mwaka 2015.
Shughuli za uokozi kwa wahamiaji kwenye mwambao wa Lampedusa, Mei 8 mwaka 2015. Reuters



Mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje wamekutana Jumatatu wiki hii mjini Brussels, Ubelgiji ili kuruhusu rasmi operesheni Navfor Med. Lengo : kukomesha wafanyabiashara wa watu kutothubutu kutumia bahari kama njia ya kufanya biashara hiyo haramu.



Hatua kali zimechukuliwa. Hatua hizo ni pamoja na kupokonya na kuharibu meli zitakazokua zikitumia katika safari hizo.
Lengo muhimu la opereshini Navfor Med ni kukomesha biashara ya watu. Operesheni hiyo inalenga pwani za Libya, ambazo zinachukuliwa kama maeneo muhimu ya biashara ya wahamiaji. Shabaha ni kutoa ulinzi kwa Bahari ya Mediterranean na kuwaokoa wahamiaji waliokua wakikabilia na ajali mbalimbali katika bahari. Lakini kwanza kupata taarifa kwa kutumia Satelaiti, rada na uchunguzi wa angani ili kutafuta njia inayotumiawa na wahamiaji.
Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuunda jeshi la pamoja la majini ili kuzuia wahamiaji haramu wanaosafirishwa barani Ulaya wakitokea nchini Libya kupitia Bahari ya Mediterranean.
Mkuu wa Mambo ya nje wa Umoja huo Federica Mogherini amesema kuwa jeshi hilo litazinduliwa rasmi mwezi ujao na makao yake makuu yatakuwa ni mjini Rome nchini Italia.
Maelfu ya wahamiaji haramu wengi kutoka barani afrika wamepoteza maisha baada ya boti walizosafiria kuzama wakiwa baharini.

Na RFI


No comments

Post a Comment