POlisi mjini Texas wamewapiga risasi watu wawili kwa kuwashambulia polisi na risasi
Polisi
mjini Texas wanasema kuwa wamewapiga risasi na kuwaua watu wawili
waliokuwa na silaha, waliowashambulia walinda usalama kwa risasi,
walipofika katika eneo la hafla moja yenye utata ya uchoraji wa vibonzo
vya kuwakejeli waislamu na mtume Mohammed.
Duru za habari zasema
kuwa kisa cha ushambuliaji wa risasi kimefanyika katika sherehe moja,
iliyokuwa ikifanyika mjini Dallas, mahala ambapo waandalizi walikuwa
wakiendesha onyesho hilo.Hafla za Sherehe hiyo iliyoandaliwa na kundi moja la kisiasa la kihafidhina, ambalo limekuwa likikejeli Uislamu, lilikuwa litoe zawadi nono ya dola milioni kumi kwa mchoraji kibonzo mahiri zaidi, atakayeibuka mshindi kwa kumchora mtume Mohamed.
Aliyeshuhudia ameiambia BBC kuwa, aliwaona maafisa wa polisi wakimtia mbaroni mshukiwa wa tatu, ambaye alionekana kuwa hana silaha.
Kikosi cha kutegua mabomu pamoja na ndege za helikopta za polisi zimefika mahali hapo kwa sasa.
No comments
Post a Comment