Monday, 4 May 2015

Wa ISRAEL wenye asili ya ETHIOPIA waandamana

Mon May 04 2015 Wa ISRAEL wenye asili ya ETHIOPIA waandamana Mamia ya wananchi wa ISRAEL wenye asili ya ETHIOPIA wam... thumbnail 1 summary
Mon May 04 2015
Wa ISRAEL wenye asili ya ETHIOPIA waandamana
Mamia ya wananchi wa ISRAEL wenye asili ya ETHIOPIA wameandamana katika mji mkuu wan chi hiyo TEL AVIV, wakipinga vitendo vya ubaguzi na ukatili vinavyofanywa na polisi wan chi hiyo dhidi yao.

Maandamano ya watu hao weusi wenye asili ya AFRIKA, yamekuja baada ya mtandao mmoja wa kijamii kuonyesha picha ya video ya askari mmoja mwenye asili ya ETHIOPIA akishambuliwa na kupigwa na askari wa ISRAEL.

Maandamano ya watu hao yalianza kwa amani, lakini ghafla yakaambatana na ghasia. Watu wenye asili ya ETHIOPIA wamepigwa marufuku nchini ISRAEL kutoa msaada wa damu.

Wizara ya afya ya nchi hiyo imesema inafanya uchunguzi kuhusiana na taarifa kuwa wanawake wenye asili ya ETHIOPIA, huchomwa sindano za uzazi wa mpango bila ridhaa yao. Waandamanaji wanasema, wote ni binadamu, hivyo wote ni sawa.

Asilimia kubwa ya waandamanaji wamezaliwa nchini ISRAEL. Wazazi wa waandamanaji hao walipelekwa nchini humo miaka ya 80, pale ISRAEL, ilipopeleka ndege maalum nchini ETHIOPIA kuwachukua watu wenye damu ya ISRAEL.

No comments

Post a Comment