Waasi wanaoiunga mkono Urusi mashariki mwa Ukrain wamewaachilia huru raia wawili wa Marekani ambao ni watoa huduma za misaada baada ya kuwazuilia kwa zaidi ya wiki mbili.
Wawili hao ni kati ya wafanyikazi 30 waliokamatwa wakati watu waliokuwa wamejifunika nyuso walipoivamia ofisi ya shirika moja la kimataifa la kutoa misaada mjini Donetsk siku kumi zilizopita.Wafanyikazi wengine waliachiliwa saa 24 baada ya kukamatwa.
Mkuu wa shirika hilo ambaye ni waziri wa zamani wa mashauri ya kigeni wa uingereza David Milband, anasema kuwa watoa huduma za kibinadamu hawastahili kulengwa . bbc may 9 2015
No comments
Post a Comment