Tue May 19 2015
Rais FILIPE NYUSSI wa MSUMBIJI
Rais FILIPE NYUSSI wa MSUMBIJI amewashauri wawekezaji na
wafanyabiashara wa TANZANIA kutumia fursa zilizopo kuwekeza nchini
MSUMBUJI.
Rais NYUSSI ametoa kauli hiyo Jijini DSM wakati wa kongamano lililohusisha wawekezaji na wafanyabiashara wa TANZANIA.
Rais huyo wa MSUMBIJI ameahidi kuwasaidia wafanyabisha na wawekezaji wa TANZANIA kupata mazingira mazuri ya uwekezaji nchini MSUMBIJI ili waweze kuendesha shughuli zao bila vikwazo nchini humo hasa katika sekta ya gesi, kilimo na usindikaji.
Rais NYUSSI pia ametoa wito kwa Watanzania kudumisha amani na utulivu hasa katika kipindi cha mwaka huu ambapo Taifa linashiriki katika uchaguzi mkuu.
No comments
Post a Comment