Tuesday 19th May 2015 / Reads: 5
KILIMANJARO
wananchi wa Wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro, hususani wale waishio
maeneo ya kuzunguka soko la Sanya juu wapo hatarini kupata magojwa ya
mlipuko ikiwamo Kipindupindu kutokana na kuuza vyakula katika mazingira
hatarishi, kufuatia soko hilo kukithiri kwa uchafu na ubovu wa
miundombinu.Wafanyabiashara wa soko hilo wakiongea na waandishi wa
habari kwa nyakati tofauti bila kutaja majina yao kwa kuhofia usalama
wao, Wafanyabiashara hao walisema kuwa wanailalamikia Halmashauri ya
Wilaya hiyo kwa madai ya kutokufanya ukarabati kwani soko hilo
linahatarisha afya za wafanyabiashara pamoja na wanunuzi wa vyakula
katika soko hilo.Mmoja wa Wafanyabiashara wa soko hilo alisema kuwa
wanapanga vyakula chini tena kwenye tope mazingira ni machafu lakini
hawana njia nyingine ya kuendesha maisha zaidi ya uendelea kufanya
biashara katika soko hilo, aliongeza kwa kusema Halmashauri inakusanya
ushuru kila ifikapo siku ya soko na hawajui fedha hizo zinatumika katika
shughuli gan?Wafanyabiashara hao walisema kuwa, soko hilo ambalo
limekuwa likitoa Viazi, Ndizi, Maharage na Maparachichi, na kusambazwa
katika masoko mbalimbali nchini ikiwamo jiji la Dar es Salaam,
linatakiwa kuwekewa miundombinu imara na mazingira kuwa safi wakati
wote.Ambapo waliseme kuwa miundombinu hiyo ni pamoja na kuwekewa Moramu
na mifereji ili kuwezesha Wananchi kupita kwa usalama pia wafanya
biashara kufanya biashara zao katika mazingira mazuri hasa kipindi hichi
cha mvua za masika, tunaomba marekebisho hayo yafanyuke mapema
iwezekanavyo kabla hatujaandamana hadi ofisi ya mkurungenzi.
Article Source: Kilimanjaro Official Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment