Wahamiaji haramu wanusurika kufa maji nchini ITALIA
Mamia ya wahamiaji haramu waliookolewa kufamaji katika bahari ya
MEDITERANIAN, baada ya mtumbwi waliokusa wakisafiria kuzama, wamewasili
katika kisiwa cha POZZALLO, nchini ITALIA.
Walinzi katika pwani ya ITALIA wanasema katika kipindi cha saa 24 zilizopita wamewaokoa watu 877, kutoka baharini waliokuwa katika hatari ya kufa maji.
Umoja wa mataifa unasema, mwaka huu ndio unaoongoza kwa idadi kubwa ya wahamiaji haramu kuokolewa katika bahari ya MEDITERANIA, huku mamia pia wakipoteza maisha.
LIBYA, pia imeomba msaada wa kimataifa kukabiliana na wahamiaji haramu, wanaoanzia safari zao kwenda barani ULAYA, katika pwani ya nchi hiyo, kwani wahamiaji hao wanaendelea kufurika.
source; tbc
No comments
Post a Comment