Wednesday, 20 May 2015

Waomba hifadhi watembea kilometa 10 kusaka hifadhi

Wed May 20 2015 Waomba hifadhi watembea kilometa 10 kutafuta hifadhi Waomba hifadhi 36 kutoka nchini BURUNDI wakiongozw... thumbnail 1 summary
Wed May 20 2015
Waomba hifadhi watembea kilometa 10 kutafuta hifadhi
Waomba hifadhi 36 kutoka nchini BURUNDI wakiongozwa na wafanyakazi kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa na vyombo vya dola wametembea umbali wa zaidi ya kilomita 10 kutoka KAGUNGA hadi kijiji cha MUKIGO wilayani KIGOMA kutafuta hifadhi.

Msafara huo ni majaribio ya kutafuta njia mbadala ya kutembea kwa miguu ili kuongeza kasi ya kuwaondoa waomba hifadhi kutoka nchini BURUNDI waliopo katika kijiji cha KAGUNGA na kudhibiti ya magonjwa ya mlipuko kijijini hapo.

Kila kukicha serikali kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya kimataifa imekuwa ikifanya kila linalowezekana ili kuhakikisha waomba hifadhi kutoka nchini Burundi waliopo katika kijiji cha KAGUNGA wilayani Kigoma wanaondolewa haraka na kupelekwa maeneo salama.

Awali afisa kutoka shirika la kimataifa linaloshughulika na masuala ya uhamaji IOM Charles Mkude ameitaja njia ya kutoka Kagunga hadi Mukigo kuwa imelenga kuongeza kasi ya kuwaondoa waomba hifadhi waliopo katika kijiji hicho

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya uratibu ya maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amesema anaimani kuwa ubunifu unaofanywa na serikali kwa kushirikiana mashirika wa kutafuta njia mbalimbali mbadala utaepusha maafa hasa magonjwa ya mlipuko katika kijiji cha KAGUNGA.

No comments

Post a Comment