Wednesday, 20 May 2015

Kipindupindu chaenea kambi za wakimbizi wa Burundi


Wimbi la wakimbizi wa Burundi wanaokimbia machafuko nchini mwao limepelekea kuzuka ugonjwa hatari wa kipindupindu katika kambi za wakimbizi hao mkoani Kigoma Tanzania.
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na asasi nyinginezo zimechukua hatua za dharura za kukabiliana na mfumuko wa ugonjwa huo. Tayari watu 15 wameshapoteza maisha yao na wengine 500 kuambukizwa maradhi hayo ambayo yanasababishwa na kutochunga usafi.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Tanzania Dk Stephen Kebwe amesema kuwa wizara hiyo kwa kushirikiana na WHO wamechukua hatua za lazima ikiwa ni pamoja na kuunda timu ya madaktari kwa ajili ya kutumwa mkoani Kigoma kukabiliana na mfumuko wa ugonjwa huo.
Naibu Waziri wa Afya wa Tanzania ameongeza kuwa, wamepeleka vifaa vinavyotakiwa huko Kigoma kama ambavyo wanathmini hali ya mambo na kuangalia uwezekano wa kuwapeleka wakimbizi wa Burundi katika mikoa mwngine iliyoko karibu na nchi hiyo kama vile Kagera, Katavi na Geita.

No comments

Post a Comment