Mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Yanga watakamilisha furaha ya ubingwa wao kwa kukabidhiwa “mwali wao” (kombe) Jumatano.
Yanga
watakabidhiwa Kombe hilo muda mfupi baada ya mechi yao ya kukamilisha
ratiba dhidi ya Azam itakayochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.Katika kunogesha furaha ya kutwa kombe hilo, Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), limesogeza muda wa kuanza kwa mechi hiyo, mpaka saa kumi na moja jioni, kutoka katika muda wa kawaida, saa 10 ili kuwapa fursa mashabiki wa klabu hiyo kuhudhuria kwa wingi baada ya kutoka katika harakati zao za maisha.
Yanga ilitwaa ubingwa ikiwa na mechi tatu mkononi kwa kuwa na pointi nyingi (550 kuliko timu yoyote.
Baada ya mechi hiyo dhidi ya Azam, Yanga itabakiwa na mechi ya mwisho dhidi ya Ndanda wakati Azam watakuwa na kibarua cha mwisho kigumu dhidi ya Mgambo, walio katika hatari ya kushuka daraja.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fennela Mkangara.
No comments
Post a Comment