Tue May 05 2015
REAL MADRID na YUVENTUS kupimana nguvu
Ligi ya mabingwa barani ulaya unafanyika mchezo mmoja wa nusu
fainali ambapo kibibi kizee cha TURIN- YUVENTUS watavaana na mabingwa
mara kumi wa ulaya wakiwa wanatetea taji lao msimu huu REAL MADRID.
Mchezo huo unafanyika katika dimba la nyumbani la YUVENTUS mjini TURIN huku wenyeji wakiwa bado wanasherehekea ubingwa wao wa NNE mfululizo wa ligi soka daraja la kwanza nchini ITALIA-SERIA A.
Kocha wa YUVENTUS-MASIMILIANO ALEGRI amejinasibu kuwa wamejipanga kuhakikisha wanafanya vyema katika mchezo wa leo pamoja na ule wa marejeano utakaofanyika juma lijalo mjini MADRID, huku kocha wa REAL MADRID, CARLO ANCELOTI akisema mipango yao ni kufuzu kwa hatua ya fainali na kujaribu kuweka rekodi mpya ya kuwa timu ya kwanza kufanikiwa kutetea taji la ligi ya mabingwa barani ulaya.
Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa katika mchezo wa makundi msimu wa 2013-2014 ambapo timu hizi zilitoka sare ya kufungana magoli MAWILI kwa MAWILI.
YUVENTUS mara ya mwisho kucheza mchezo wa nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani ulaya ilikuwa miaka 12 iliyopita ambapo walifanikiwa kufuzu kwa hatua ya fainali, na kwa sasa wanajivunia rekodi yao safi yta kutofungwa michezo 12 ya ligi ya mabingwa barani ulaya katika uwanja wao wa nyumbani.
Mechi nyingine ya ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya nusu fainali itafanyika kesho katika dimba la NOU CAMP ambapo wenyeji FC BARTHELONA watakuwa wenyeji wa BAYERN MUNICH.
Mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja na televisheni yako ya TBC 2 kuanzia saa 4 kasorobo usiku.
No comments
Post a Comment