Hakuna njia nyingine ila kusonga mbele nchini Burundi katika harakati za
kuitekeleza katiba ya nchi.Hayo anasema mwandishi wetu Claus Stäcker
katika maoni yake.
Rais Pierre Nkurunziza ambae hapo awali alikuwa kiongozi wa waasi kwa
mara nyingine amethibitisha kwamba yeye ni kamanda hodari wa
kijeshi.Amefanikiwa kuwazuia wanajeshi waasi kumwondoa madarakani. Na
jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki imeshikamana naye katika kipindi
chake kigumu.
Waziiri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe amesema bara la Afrika
halitaki kumwona kiongozi anaetwaa mamlaka ya nchi kwa kutumia nguvu za
kijeshi. Umoja wa Afrika pia ulililaani jaribio la kumwondoa Nkurunziza
madarakani. Umoja wa Afrika umelishutumu jaribio la wanajeshi la kutaka
kutwaa mamlaka kwa njia ya mabavu.
Kauli hizo zingekuwa za kutia moyo laiti bara lote la Afrika lingekuwa
mahala penye viongozi wenye imani za kidemokrasia. Kutokana na viongozi
wengi kuyadumisha mamlaka yao kwa njia ya mabavu, Umoja wa Afrika mara
nyingi unakaukiwa sauti.
Mfano ni Mmenyekiti wa sasa wa Umoja huo ,Robert Mugabe wa
Zimbabwe.Hakuna taasisi yoyote ya kiafrika iliyothubutu kuzizuia sera za
Mugabe zinazoenda kinyume na misingi ya deomkrasia..
Rais Pierre Nkurunziza ni mshindi alieshindwa
Wapo viongozi watano barani Afrika, mashariki na magharibi mwa bara hilo
wasiotaka kuondoka madarakani kwa hiari zao.Na Rais Nkurunziza wa
Burundi ni miongoni mwa viongozi hao.
Mpaka sasa bado hajaweza kuzisoma alama za nyakati. Na licha ya
kufanikiwa kurejea nyumbani baada ya jaribio la wanajeshi la kutaka
kumwondoa madarakani, yeye bado hajawa mshindi.
Nukurunziza amewatishia wanasheria,wanasiasa na waandishi wa habari.
Polisi wake wamewapiga risasi raia. Baada ya miaka 10 ya kuchukua hatua
za busara katika kurejesha utulivu nchini, Nkurunziza amechapuka na
kuicha njia ya maridhiano,ujenzi mpya wa nchi na kujenga demokrasia.
Rais Nkurunziza ameirudisha Burundi katika enzi za kijeshi. Amelijenga
jeshi la vijana linalowatishia watu nchini, kwa niaba yake ili aweze
kuhakikisha kwamba anachaguliwa tena. Vijana hao wanawatisha siyo tu
washindani wa kisiasa bali pia wanavunja miiko: kwa kuwashutumu Watutsi
kwa kula njama. Mvutano wa kikabila unaweza kuwa hatari kubwa sana kwa
Burundi.
Njama hizo zinakumbusha yale yaliyotokea kati ya mwaka wa 1993 na 2000.Vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hakuna njia nyingine nchini Burundi ila ile ya kusonga mbele na harakati
za kuitekeleza katiba .Nkurunziza anaweza kuleta mabadiliko makubwa
nchini Burundi ikiwa ataachana na mpango wa kuwania muhula wa tatu wa
urais.
Tuesday, 19 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment