Mjumbe
wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amesema
ikiwa hatua ya kuondoa majeshi ya Burundi itafanyika nchini Somalia
itaathiri mapambano dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab.
mwanzoni mwa
juma hili Marekani ilitangaza kupunguza kiasi cha pesa inachotoa kwa
majeshi ya Burundi baada ya shutuma kuwa jeshi hilo limejihusisha katika
vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadam wakati wakizima vurugu
zilizojitokeza wakati jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Rais
Pierre Nkurunziza liliposhindwa.AU nayo imesita kupeleka kundi jingine la wanajeshi wa Burundi nchini Somalia.Lakini Kay ameiambia BBC kuwa majeshi ya Umoja wa Afrika yanahitaji msaada kuweza kupambana na Al Shabaab.pia ametahadharisha kuongezeka kwa mahitaji ya kibinaadam nchini Somalia na kutoa wito wa jumuia ya kimataifa kuendelea kupeleka misaada nchini humo.
No comments
Post a Comment