Monday, 18 May 2015

Iran: Ripoti ya UN kuhusu Iran ni bandia

Iran imekosoa ripoti ya hivi karibuni ya ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa aliyedai kuna ongezeko la hukumu za kifo nchini. Katika ta... thumbnail 1 summary
Iran imekosoa ripoti ya hivi karibuni ya ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa aliyedai kuna ongezeko la hukumu za kifo nchini.

Katika taarifa, Idara ya Haki za Binadamu Katika Vyombo vya Mahakama Iran imeikosoa ripoti hiyo na kusema imejengeka katika msingi wa taarifa ghalati na vyanzo bandia. Idara hiyo imewataka maafisa wa Umoja wa Mataifa kuacha kuingiza masuala ya kisiasa katika kadhia ya haki za binaadamu. Aidha taarifa hiyo imesema vyombo vya mahakama Iran vimejengeka katika msingi wa uadilifu. Hivi karibuni msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bi. Marzieh Afkham alisema Tehran inauangalia kwa shaka kubwa utendaji wa ripota maalumu wa haki za binadamu kuhusiana na Iran kutokana na kutozingatia misingi na vipimo vya kimataifa.

No comments

Post a Comment