Meli ya ulinzi ya kivita ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ipo katika Ghuba ya Aden imezionya vikali meli na ndege za kivita za Marekani kukaribia eneo la karibu na meli hiyo. Kwa mujibu wa habari, ndege mbili za doria na upelelezi za Marekani aina ya P3C na meli ya kijeshi aina ya DDG81, hazikuheshimu masafa ya umbali wa kisheria ambao ni maili tano kutoka eneo ilipokuwa meli ya doria namba 34 ya jeshi la majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ghuba hiyo ya Aden na hivyo kukapelekea kutolewa amri kali kabla ya meli na ndege hizo za Marekani kuondoka eneo hilo mara moja. Kanali wa jeshi la wanamaji wa meli hiyo ya Iran, Tajud-Din amesema kuwa meli hiyo ipo eneo hilo katika kufuatilia meli za kivita za adui zinazohatarisha usalama wa taifa la Iran katika maji ya kimataifa. Aidha ameashiria jinai za utawala wa Saudi Arabia nchini Yemen, na kusema kuwa kuwepo kwa meli za kivita za adui katika maji hayo, hakuna lengo jingine ghairi ya kutoa uungaji mkono na msaada kwa Saudia katika kubariki jinai zao nchini Yemen, hivyo uwepo wa meli za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika maji ya Ghuba ya Aden, ni kikwazo kikubwa kwa muungano huo wa adui. Inaelezwa kuwa, meli za kivita za Iran zilikuwa zimeanzisha doria mwezi mmoja kabla katika eneo la Ghuba ya Aden na lango la Babul-Mandab. Marekani ilipeleka meli zake za kivita karibu na Yemen baada ya Saudi Arabia kuanzisha mashambulizi yake ya kichokozi dhidi ya watu wa nchi hiyo.
Wednesday, 6 May 2015
Iran yaionya manuari ya kivita ya Marekani

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment