KLABU ya Yanga imesema inatarajia kufanya usajili wa wachezaji wazuri wa kimataifa kwa ajili ya kukisaidia timu yao ya soka kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema wataangalia wachezaji wengine wazuri ambao watasaidia sio tu katika michuano ya kimataifa, bali ikiwezekana kutetea taji hilo kwa msimu ujao.
Muro alisema hawatarajii kufanya usajili wa wachezaji kutoka Simba kwani wamejifunza kutokana na makosa. “Usajili tutafanya kwa wachezaji wengine wa kimataifa hivyo hatutarajii uongozi wetu utasajili wachezaji kwa watani zetu Simba, hata kama ni mzuri kwa kiasi gani au ni malaika, hatutafanya wala hatutarajii,” alisisitiza Muro.
No comments
Post a Comment