Wednesday, 6 May 2015

Wanajeshi wawili wa Tanzania wauawa DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelaani vikali shambulizi la waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambalo limeu... thumbnail 1 summary
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelaani vikali shambulizi la waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambalo limeuwa wanajeshi wawili wa umoja huo ambao wanatoka Tanzania.
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakifanya doria Mashariki mwa Kongo Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakifanya doria Mashariki mwa Kongo
Shambulizi hilo lilifanywa Jumanne jioni katika kijiji cha Kisiki, umbali wa km 38 Kaskazini mwa mji wa Beni. Mbali na wanajeshi wawili waliouawa na 13 ambao walijeruhiwa, wengine wapatao 4 hawajulikani walipo.
Wanajeshi wa Tanzania ambao ni sehemu ya kikosi maalumu cha kuingilia kati walikuwa wakifanya doria walipofanyiwa shambulizi hilo na watu wanaoaminika kuwa waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) kutoka Uganda.
Umoja wa Mataifa walaani shambulizi hilo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema Katibu Mkuu huyo amesikitishwa sana na shambulizi hilo, na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea na juhudi zake za kuhakikisha usalama wa wakazi wa Mashariki mwa Kongo wanaokabiliwa na vitisho vya waasi.
Shambulizi hilo la jana Jumanne lilikuwa la pili kufanywa dhidi ya Umoja wa Mataifa nchni Kongo katika muda wa saa 48, kwani, siku moja kabla, helikopta iliyokuwa imembeba mkuu wa kijeshi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, ilishambuliwa na watu ambao bado hawajatambuliwa.

No comments

Post a Comment