Fri May 15 2015
Kocha wa REAL MADRID akataa kuzungumzia hatma yake
KOCHA wa klabu ya REAL MADRID, CARLO ANCELOTTI amekataa
kuzungumzia mustakabali wake kufuatia kikosi chake kutolewa katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa barani ULAYA
MADRID ilishindwa kuyapindua matokeo ya kufungwa magoli MAWILI kwa MOJA katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya JUVENTUS baada ya kujikuta wakipata sare ya kufungana goli MOJA kwa MOJA.
JUVENTUS itacheza na BARCELONA katika mchezo wa fainali utakaochezwa Juni SITA mwaka huu katika Uwanja wa Olimpiki uliopo katika mji wa BERLIN, UJERUMANI.
Mara ya mwisho Juventus kutinga fainali ya michuano hiyo ilikuwa mwaka 2003 na kufungwa na AC MILAN.
No comments
Post a Comment