Friday, 15 May 2015

Rais PIERRE NKURUZINZA kuhutubia taifa

Fri May 15 2015 Rais PIERRE NKURUNZIZA Mgogoro wa kisiasa nchini BURUNDI umechukua sura mpya baada ya viongozi watatu wa j... thumbnail 1 summary
Fri May 15 2015
Rais PIERRE NKURUNZIZA
Mgogoro wa kisiasa nchini BURUNDI umechukua sura mpya baada ya viongozi watatu wa jaribio la mapinduzi ya kumwondoa madarakani Rais PIERRE NKURUNZIZA kushindwa na hatimaye kukamatwa.

Taarifa ya Ikulu ya BURUNDI imesema kiongozi wa jaribio hilo la mapinduzi Jenerali GODEFROID NIYOMBARE ametoroka na anatafutwa na wanajeshi watiifu kwa Rais NKURUNZIZA.

Awali Jenerali NIYOMBARE alisema kuwa yeye pamoja na viongozi wengine wa jaribio la mapinduzi watajisalimisha kwa wanajeshi watiifu kwa Rais PIERRE NKURUNZIZA.

Rais PIERRE NKURUNZIZA amesema tayari amewasili nchini BURUNDI na anatarajiwa kulihutubia taifa.

Hata hivyo milio ya risasi na mabomu bado inasikika katika maeneo kadhaa nchini BURUNDI licha ya kushindwa kwa jaribio hilo la mapinduzi.

Jaribio hilo limefanyika wakati Rais PIERRE NKURUNZIZA alikuwa TANZANIA akihudhuria mkutano wa mazungumzo ya amani kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini BURUNDI.

Wanajeshi watano wameuawa jana katika mapigano kwenye Mji Mkuu wa BURUNDI, BUJUMBURA.

Zaidi ya watu ISHIRINI wamekufa huku maelfu ya raia wa BURUNDI wakikimbilia nchi jirani ikiwemo TANZANIA tangu kuanza kwa ghasia za kupinga mpango wa Rais PIERRE NKURUNZIZA wa kutaka kugombea urais kwa awamu, hatua ambayo ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Mahakama ya Katiba ya BURUNDI imepitisha uamuzi wa kumruhusu Rais PIERRE NKURUNZIZA kugombea urais kwa awamu ya tatu.
tbc, mei 15 2015

No comments

Post a Comment