Tuesday, 5 May 2015

Ndege iliyosheheni chakula cha msaada yashambuliwa nchini YEMEN

Tue May 05 2015 Ndege iliyosheheni chakula cha msaada yashambuliwa nchini YEMEN Ndege iliyokuwa imesheheni misaada mbal... thumbnail 1 summary
Tue May 05 2015
Ndege iliyosheheni chakula cha msaada yashambuliwa nchini YEMEN
Ndege iliyokuwa imesheheni misaada mbalimbali kwa ajili ya waathirika mapigano yanayoendelea nchini YEMEN, imeshambuliwa na ndege za kijeshi inazosemekana ni za serikali ya SAUDI ARABIA, mjini SANAA.

Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa SANAA, wanasema ndege hiyo ilikuwa ikijiandaa kuelekea katika maeneo ya pembezoni nchini YEMEN kupeleka chakula na maji kwa watu walioathiriwa na mapigano.

Serikali ya SAUDI ARABIA, imesema inajadiliana na pande zinazoshiriki katika mapigano nchini YEMEN, kutiliana saini mkataba wa kusitisha mapigano, ili chakula kiwafikie watu walioko katika maeneo ya pembezoni.

Ushirika wa majeshi ya nchi za kiarabu yakiongozwa na SAUDI ARABIA umekuwa ukifanya mashambulio dhidi ya wapiganaji wa kikundi cha HOUTHI, walioteka maeneo mengi nchini YEMEN, kuanzia mwezi Machi.

Wakati huo huo nchini ya SENEGAL imesema itapeleka askari wake nchini YEMEN kwenda kuyasaidia majeshi ya SAUDI ARABIA, yanayojaribu kuwadhibiti wapiganaji wa kikundi cha HOUTHI.

No comments

Post a Comment