Wednesday, 6 May 2015

Ndege za kivita zashambulia Yemen

Ndege za kivita za muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia zimefanya zaidi ya mashambulizi 30 usiku wa kuamkia leo, kaskazini-maghar... thumbnail 1 summary
Ndege za kivita za muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia zimefanya zaidi ya mashambulizi 30 usiku wa kuamkia leo, kaskazini-magharibi mwa Yemen kwenye majimbo ya Saada na Hajja, mpakani na Saudi Arabia.
Moja ya ndege zilizoharibiwa kufuatia mashambulizi ya angani yanayoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya uwanja wa ndege wa Sana'a. Moja ya ndege zilizoharibiwa kufuatia mashambulizi ya angani yanayoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya uwanja wa ndege wa Sana'a.
Maafisa wa Yemen wamesema mashambulizi hayo ya anga yamefanywa kwenye mji wa mpakani wa Najran ulio umbali wa kilomita tatu kutoka kwenye mpaka wa Yemen, baada ya waasi wa Houthi nchini Yemen kurusha makombora na roketi jana, yaliyoharibu shule moja ya wasichana na hospitali.
Hilo ni shambulizi la kwanza kufanywa na waasi hao katika eneo la Saudi Arabia, tangu muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ulipoanzisha operesheni ya kijeshi dhidi ya waasi hao Machi 26, mwaka huu. Kwa mujibu wa maafisa hao, mashambulizi hayo ya makombora yalikuwa yakifanywa kutoka kwenye mpaka wa Saudi Arabia.
Waasi wa Houthi Waasi wa Houthi
Eneo la Saada ni ngome muhimu kwa waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran. Duru za waasi hao zimeeleza kuwa raia 43 wameuawa na wengine wapatao 100 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ambayo yamefanyika hadi leo alfajiri. Hata hivyo idadi hiyo bado haijathibitishwa. source bbc Swahili, mei 6 2015

No comments

Post a Comment