Kutokana na hali ya mgomo ulioendelea Chuo
kikuu cha Dodoma siku ya juzi na jana tayari umeacha athari nyingi katika jamii
ya UDOM, ikiwemo sekta ya kiroho. Mahahafali ya kuwaaga mwaka wa tatu Chuo
kikuu cha Dodoma imeahirishwa na kusogezwa mbele baada ya hali ya amani kupotea
kwa muda kadhaa katika chuo hicho. Tegemeo la wote ikizungumza na Mwenyekitii
mstaafu Mtumishi wa Mungu Bw. Thomas Masanja aliyekuwa Mwenyekiti wa USCF
(University Students Christian Fellowship) kikundi cha kikristo kinachobeba
wanachuo waamini wa makanisa ya CCT nchini likiwemo Anglican, Morovian,
Lutherani-KKKT na Baptist church alisema, “mahafali imesogezwa kutoka siku ya
leo jumamosi tarehe 23 mwezi huu wa tano na tutaifanya jumamosi ijayo ya tarehe
30, mwezi huu. Wito wangu kwa jamii ni kuwa wawajibikaji wazuri katika nafasi
zetu tulizonazo kwenye jamii, kila mtu atimize wajibu wake kwa muda
unaotakiwa”. Meseji nyingi zimetumwa kutoka kwa waumini na wahitimu wa USCF
kwenda kwa marafiki zao ili kuwataarifu juu ya kusogezwa kwa sherehe hii.
Saturday, 23 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment