Saturday, 23 May 2015

WALIOKACHA DEPO-JKT KUSAKWA

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga... thumbnail 1 summary
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein MwinyiWAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2013/14, 2014/15 na kutojiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) bila ridhaa ya jeshi hilo, wanaendelea kusakwa na kuorodheshwa kwenye orodha ya watoro na upo uwezekano wa wao kwenda mafunzo hayo mapema mwezi ujao.
Akiwasilisha hotuba ya wizara hiyo bungeni jana ya Makadiro ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka 2015/16, Dk Mwinyi alisema mafunzo ya JKT kwa wahitimu hao hutolewa kwa mujibu wa Sheria, ambapo ni ya kuwajengea uzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa na kutoa stadi za kazi.
Alisema kwa mwaka 2014/15 jumla ya vijana waliopata mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria ni 31,635 ambayo ni sawa na ongezeko la vijana 15,632, ukilinganisha na vijana 16,003 waliohitimu mafunzo hayo mwaka 2013/14 .

No comments

Post a Comment