Thursday, 7 May 2015

Mgomo wa matreni Ujerumani kuendelea hadi Jumapili

Kiongozi wa chama cha madereva wa matreni hapa Ujerumani - GDL amesema leo kuwa mgomo wao wa siku saba utaendelea na akapinga pendekezo la h... thumbnail 1 summary
Kiongozi wa chama cha madereva wa matreni hapa Ujerumani - GDL amesema leo kuwa mgomo wao wa siku saba utaendelea na akapinga pendekezo la hivi punde la kampuni ya huduma za treni ya Deutsche Bahn la mwaliko kwa ajili ya mazungumzo ya kutatua mgogoro huo kuhusu malipo na haki nyingine. Claus Weselsky ameliipuzilia mbali pandekezo hilo akisema wamelitathmini na kuliona lisilokuwa la maana hivyo basi mgomo wao utaendelea hadi siku ya Jumapili. Chama cha GDL kilianzisha mgomo huo wa siku saba Jumatatu wiki hii ili kudai nyongeza ya mshahara ya asilimia 5 na kupunguzwa kwa muda wa kufanya kazi kwa wiki, kutoka saa 39 hadi 37 pamoja na kufanya mazungumzo kwa niaba ya wafanyakazi wengine wa reli kama vile wahudumu wa ndani ya treni.

No comments

Post a Comment