Friday, 8 May 2015

MSUVA amchefua PLUIJM

Kocha huyo alisema anashangazwa na kitendo cha kinara huyo wa mabao wa Ligi Kuu ya Bara kutimkia nchini Afrika Kusini bila kuaga na kudai h... thumbnail 1 summary
Kocha huyo alisema anashangazwa na kitendo cha kinara huyo wa mabao wa Ligi Kuu ya Bara kutimkia nchini Afrika Kusini bila kuaga na kudai huo ni utovu wa nidhamu.
SHARE THIS STORY
HUENDA kiu ya kutaka kucheza soka la kulipwa ndilo lililomfanya winga wa Yanga, Simon Msuva kuamua kutoroka kwenda Afrika Kusini bila ya ruksa ya uongozi, lakini jambo hilo limemkera kocha Hans Pluijm.

Kocha huyo alisema anashangazwa na kitendo cha kinara huyo wa mabao wa Ligi Kuu ya Bara kutimkia nchini Afrika Kusini bila kuaga na kudai huo ni utovu wa nidhamu.

Msuva mwenye mabao 17 ametimkia Sauzi ili kufanya majaribio kwenye klabu ya Orlando Pirates inayoshiriki Ligi Kuu iliyowahi pia kutoa mastaa waliotamba duniani kama Sibusiso Zuma, Benni McCartthy na Lucas Radebe.

Pluijm aliliambia Mwanaspoti kuwa, Msuva hakufanya kitendo cha kiungwana kuondoka bila ruhusa ya uongozi wa Yanga na yeye anakichukulia kama utovu wa nidhamu.

“Alinifuata akiwa tayari na tiketi akiniambia anataka kwenda Afrika Kusini, nikamsihi asifanye hivyo hadi uongozi umruhusu. Nashangaa kusikia ameondoka, kwa kweli sijapendezwa na jambo hilo,” alisema Pluijm.

Pluijm alisema kuwa Msuva hakuwahi kuwa na ugomvi wowote na Yanga. hivyo alipaswa kufuata taratibu kabla ya kuelekea nchini humo kujaribu bahati yake.

Wakati huohuo mshambuliaji Mrisho Ngassa amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Free State Stars ya nchini Afrika Kusini.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti inazo kutoka kwa mtu wa karibu na mchezaji huyo, zinasema kuwa mchezaji huyo atajiunga na timu hiyo rasmi mwezi Julai.

“Ngassa amesaini mkataba wa miaka mitatu Freestate inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini. Iwapo mambo yataenda sawa atajiunga nao rasmi mwezi wa saba,” kilisema chanzo hicho.

Mshambuliaji huyo ni miongoni wa wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwa kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa msimu huu.

No comments

Post a Comment