Friday, 8 May 2015

YANGA YAONGEZA WABONGO WAWILI

Safari hii ipo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na bado inaendelea na ushiriki wa Ligi ya ndani. Yanga tayari imeshawahi nafasi ... thumbnail 1 summary
Safari hii ipo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na bado inaendelea na ushiriki wa Ligi ya ndani. Yanga tayari imeshawahi nafasi kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika na kwa mujibu wa CAF ni timu nne tu za Afrika zimejihakikishia kupanda ndege mwakani mpaka sasa.
SHARE THIS STORY
0
Share
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haijawahi kukosa kutia mguu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa miaka nane mfululizo tangu mwaka 2007 mpaka dakika hii unavyosoma hapa.
Safari hii ipo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na bado inaendelea na ushiriki wa Ligi ya ndani. Yanga tayari imeshawahi nafasi kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika na kwa mujibu wa CAF ni timu nne tu za Afrika zimejihakikishia kupanda ndege mwakani mpaka sasa.
Kati ya hizo imo Yanga, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Telecom ya Djibout na Lioli ya Lesotho. Nchi za Tunisia, Misri, Congo DR, Algeria, Sudan, Ivory Coast, Morocco, Cameroon, Congo Brazavile, Mali, Nigeria na Afrika Kusini ndio pekee zinazoruhusiwa kuingiza timu mbili kila moja kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na viwango vya ubora wa soka.
Hivyo Yanga pia itasubiri tu majina lakini lazima nchi hizo zishiriki. Yanga wameshtukia dili na kuanza kuisuka timu hiyo mapema kwa kufuata matakwa ya kocha Hans Pluijm ambaye Mwanaspoti linajua kwamba kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachosema kwamba akiingiliwa tu kwenye usajili asepe zake na fidia alipwe.
Yanga baada ya kumshusha kiungo Msierra Leone, Lansana Kamara ambaye inasubiri aanze majaribio, imeanza mazungumzo ya awali ya kusajili vifaa viwili vya Friends Rangers, ambao ni beki Samwel Nkomola pamoja na kiungo Musa John.
Habari kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, zinasema kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans Van der Pluijm ameagiza kwamba baada ya kumaliza mechi na Ndanda kesho Jumamosi, ameomba wacheze mechi ya kirafiki na Friends Rangers ili ajiridhishe na vijana hao baada ya kuwaona awali katika Ligi Daraja la Kwanza.
“Kocha ameomba ichezwe mechi ya kirafiki na timu hiyo, lengo ni kuwaona wachezaji ambao anawataka kwa ajili ya kuwaongeza katika kikosi cha msimu ujao, tukimaliza mechi ndipo tutakapopanga ni lini tutacheza,” alisema mmoja wa vigogo mwenye ushawishi kwenye usajili wa Yanga.
Katibu wa Friends Rangers, Herry Mzozo alikiri kupokea ombi hilo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Yanga, kuwahitaji wachezaji hao na pia kucheza nao mechi ya kirafiki.
“Ni kati ya wachezaji ambao wameonyesha uwezo wa hali ya juu katika michuano ya Ligi Daraja la Kwanza ambayo hatukufanikiwa kufikia malengo yetu,” alisema kiongozi maarufu kwa kukuza wachezaji wengi mchangani waliosajiliwa na timu kubwa.
Pia alisema timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, zimeomba ofa kwa baadhi ya wachezaji lakini kinachosubiriwa ni wamalize mechi kwanza ndipo mazungumzo yaanze na wao wajue wanatoa wachezaji wangapi ili wapate idadi ya kuwaongeza watakaosaidia kuhakikisha kikosi hicho kinapanda msimu ujao.

No comments

Post a Comment