Friday, 8 May 2015

MWINYI ATIMIZA MIAKA 90, shikamoo Mwinyi.

Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi maarufu kwa jina la ‘Mzee Ruksa’ leo anatimiza miaka 90. Bado ana nguvu, mchangamfu, mcheshi na a... thumbnail 1 summary
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi maarufu kwa jina la ‘Mzee Ruksa’ leo anatimiza miaka 90. Bado ana nguvu, mchangamfu, mcheshi na anapopata fursa, anawafundisha Watanzania matumizi ya Kiswahili Sanifu na kutoa ushauri juu ya umuhimu wa elimu na kuishi kwa amani na ushirikiano bila ubaguzi kwa misingi ya dini na ukabila.
Alhaj Mwinyi aliyeingia madarakani kuiongoza Tanzania  Novemba 5, 1985, alizaliwa Mei 8, 1925 huko Kivule wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, tarehe ya kuzaliwa kwake ina utata kutokana na baadhi ya kumbukumbu kuonyesha kuwa alizaliwa Mei 8, huku tovuti rasmi ya Ikulu ikionyesha kwamba alizaliwa Mei 5.
Elimu
Alhaj Mwinyi alianza safari yake kielimu huko visiwani Zanzibar ambako alisoma katika Shule ya Msingi Mangapwani mwaka 1933 hadi 1936. Baadaye  alijiunga na Sekondari ya Dole mwaka 1937 hadi 1942, kisha alijiunga na Chuo Cha Ualimu Zanzibar mwaka 1943 hadi 1944.
Baada ya kuhitimu ualimu kati ya mwaka 1945 hadi 1950 alirudi  Mangapwani safari hii siyo kusoma, bali kufundisha. Mwaka 1950 alipandishwa cheo akawa Mwalimu Mkuu katika shule hiyo hadi mwaka 1954.
Mwinyi hakuwa mtu wa kuridhika na elimu aliyonayo hivyo, akiwa kazini, alikuwa akijiongezea elimu kwa njia ya posta na kuhitimu ‘General Certificate in Education’ (GCE). Pia, alisoma kwa njia ya posta na kuhitimu Stashahada ya Ualimu katika Taasisi ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Durban, Uingereza.
Mwaka 1956 Mwinyi aliajiriwa kuwa mkufunzi katika Chuo Cha Ualimu Zanzibar kazi aliyoifanya hadi mwaka 1961. Baadaye alijiunga tena na Taasisi ya Regent ya London, Uingereza ambako alisoma kwa njia ya posta na kuhitimu  cheti cha ufundishaji Lugha ya Kiingereza.
Mwaka huohuo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Hall, Uingereza na kusomea kozi ya ufundishaji (Tutors’ Attachment Course) hadi mwaka  1962. Mwinyi pia ana cheti ya Lugha ya Kiarabu alichokipata kwa kusoma Cairo, Misri kati ya mwaka 1972 na 1974.
Kwa hiyo, Mwinyi ni mwalimu aliyekamilika. Alipojitosa katika siasa na kupewa nafasi mbalimbali za uongozi, ni kama alikuwa amebadilisha darasa kutoka lile lenye kuta ambalo huwa na wanafunzi kati ya 24 na 45, wakati ule, hadi nchi nzima kuwa darasa na wananchi kugeuka kuwa wanafunzi.
Kazi na siasa
Mwaka 1964, akiwa na umri wa miaka 39, Mwinyi alianza rasmi harakati za kisiasa; alijiunga na Chama cha Afro Shiraz (ASP) huko Zanzibar. Umahiri wake katika kujenga hoja, ushawishi wake na mvuto kisiasa vilimwezesha kukitumikia chama katika ngazi na nafasi mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Kati ya mwaka 1964 na 1965 alishika wadhifa wa katibu mkuu wa muda katika Wizara ya Elimu kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Biashara Zanzibar – Zanzibar State Trading Corporation (ZSTC), mwaka 1965 hadi 1970. mwananchi

No comments

Post a Comment