Tuesday, 19 May 2015

Vyama vya siasa vyatakiwa kutopotosha umma

Tue May 19 2015 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC- Jaji DAMIANI LUBUVA Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchag... thumbnail 1 summary
Tue May 19 2015
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC- Jaji DAMIANI LUBUVA
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC- Jaji DAMIANI LUBUVA amewataka baadhi ya wananasiasa hapa nchini kuacha kupotosha wananchi kuhusiana na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwamba utaahirishwa na badala yake wananchi waendelee kujitokeza na kujiandikisha.

Jaji LUBUVA amesema hayo alipofanya ziara ya kutembelea baadhi ya kata za Manispaa ya MTWARA MIKINDANI mkoani MTWARA kuangalia mwenendo mzima wa zoezi la uandikishaji daftari la wapiga kura linavyoendelea kufanyika mkoani MTWARA na kuwataka wananchi kutokuwa na mashaka juu ya kauli hizo za baadhi ya wanasiasa ambao wanaingilia kazi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Jaji Lubuva amevitaka vyama hivyo vya siasa kuwaeleza wananchi sera zao badala ya kuingilia kazi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Limbakisye Shimwela,amesema kwa ujumla zoezi linaenda vizuri katika Manispaa hiyo na wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi.

No comments

Post a Comment