WASIFU
Umri: Miaka 67
Elimu: Shahada ya Sheria (L LB) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kazi: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Na Julius Mtatiro
Mnamo mwaka 1995, Pinda alijaribu
kugombea ubunge katika Jimbo la Mpanda Mashariki lakini alishindwa
katika hatua ya kura za maoni na ikampasa kurejea kwenye kazi yake ya
awali Ikulu.
Mizengo Pinda alizaliwa Agosti 12, 1948 mkoani
Rukwa (atafikisha miaka 67 Agosti mwaka huu).
Pinda ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 2008.
Pinda ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 2008.
Wazazi wa Mizengo Pinda wote walikuwa wakulima kwa
hiyo kijana pia alifuata nyayo hizo huku akifanya jitihada kubwa kwenye
masomo yake na kufanikiwa kuhitimu shule ya msingi na sekondari,
akifaulu vizuri kila alikopita.
Baada ya masomo yake ya sekondari, Pinda alijiunga
na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea Shahada ya Sheria (LLB) mwaka
1971 hadi 1974. Baada ya kuhitimu, alijiunga katika utumishi kwenye
Wizara ya Sheria akiwa Mwanasheria wa Serikali na alikaa katika utumishi
huo tangu mwaka 1974 hadi 1978.
Mwaka 1978, alifanya kazi akiwa “Ofisa Usalama wa
Taifa” akiwa Ikulu hadi mwaka 1982, Rais wakati huo, Mwalimu Julius
Nyerere alipomteua kuwa katibu wake binafsi (Katibu wa Rais) nafasi
aliyoishikilia hadi mwaka 1985.
Baada ya Mwalimu Nyerere kung’atuka na kuikabidhi
nchi kwa Ali Hassan Mwinyi, Pinda alitakiwa kubaki kuendelea kumsaidia
Mzee Mwinyi na alikubali wito huo. Akaendelea kuitumikia Ikulu chini ya
utawala wa Mwinyi hadi mwaka 1992.
Mnamo mwaka 1995, Pinda alijaribu kugombea ubunge
katika Jimbo la Mpanda Mashariki lakini alishindwa katika hatua ya kura
za maoni na ikampasa kurejea kwenye kazi yake ya awali Ikulu.
Baada ya Mkapa kuteuliwa kurithi Ikulu mwaka 1995,
alimteua Pinda kuwa karani wa Baraza la Mawaziri. Wadhifa alioushikilia
kuanzia mwaka 1996 hadi 2000.
Pinda amemuoa Tunu na wamepata watoto wanne; Janet, Jenifer, Hardwick na Narusi.
Mbio za ubunge
Mwaka 2000, Pinda aliachana na utumishi ndani ya
Serikali na Ikulu akajitupa jimboni Katavi kusaka ubunge kwa mara
nyingine, safari hii alipita ndani ya kura za maoni za CCM akafanikiwa
kuwashinda wapinzani na kuwa mbunge.
Nyota ya Pinda ilizidi kung’ara mwaka 2001, pale
Rais Mkapa alipomteua kuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (Tamisemi) akifanya kazi chini ya waziri wake, Brigedia
Jenerali Hassan Ngwilizi, hadi mwaka 2005.
No comments
Post a Comment