Wednesday, 6 May 2015

Wimbi la wakimbizi wa Burundi katika nchi za Rwanda, Tanzania na Kongo

Maelfu ya raia wa Burundi wanaendelea kukimbilia katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda kutokana na ghasia na machafujo y... thumbnail 1 summary
Maelfu ya raia wa Burundi wanaendelea kukimbilia katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda kutokana na ghasia na machafujo yanayoendelea nchini humo. Maafisa wa serikali ya Kongo wanasema kuwa hadi sasa wakimbizi elfu 7 wa Burundi wamevuka mpaka ya kuingia katika mji wa Uvira huko mashariki mwa Kongo. Wakimbizi hao wanasema wafuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD wametishia kuwaua iwapo hawatampigia kura Rais wa sasa wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza katika uchaguzi ujao. Baadhi ya wanafunzi waliokimbia nchi wakiwa pamoja na jamaa zao pia wamesema vijana wa chama tawala wanakwenda mashuleni kwa ajili ya kusajili majina ya wanafunzi wanaotaka kujiunga na kambi za mafunzo ya kijeshi.

No comments

Post a Comment